Kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Mwanza inayosikiliza Kesi namba 11 ya Usafirishaji haramu wa Binadamu inayomkabili Diana Bundala maarufu Zumaridi, Leo Sep 09 , 2022 imeshindwa kuendelea kutokana na upande wa Jamhuri kushindwa kukamilisha upelelezi wa kesi hiyo kwa zaidi miezi nane, ambapo Hakimu Mkazi Mfawidhi Monica Ndiyekobora anayoisikiliza kesi hiyo ameiahirisha na itatajwa tena Sept 23, 2022.