October 09 2015 kuna tukio lilitokea linalomhusisha kijana Benedicto Ngonyani ambaye alituhumiwa kusambaza ujumbe ambao ulichukuliwa kama ni uzushi na kinyume cha sheria ya makosa ya mtandao.
Ujumbe huo ambao ulisambaa kwenye mitandao ya kijamii ulikuwa ukisema kwamba Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Luteni Jenerali Davis Mwamunyange amepewa sumu, suala hili lilipelekea kijana huyo kukamatwa na kupelekwa rumande.
Ayo TV imezungumza na wakili wa Benedict Ngonyani, Edward Kikuri ambaye ameeleza kesi hiyo ilipofikia hadi sasa ………
>>>’kesi imesimama kisutu kwa sababu jalada halipo, lipo Mahakama Kuu na sisi mawakili wa upande wa utetezi hatujapata wito wowote wa kuendelea na rufani hiyo isipokuwa mawakili wa serikali huwa wanaiambia mahakama kwamba kesi ya rufani au ya kupinga kupewa rufani ipo tayari mahakama kuu‘
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.
ULIIKOSA YA MAFURIKO MIKUMI JIMBONI KWA PROF JAY? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI