Michezo

Yaliyojiri katika kesi ya Oscar Pistorius kumuua mpenzi wake

on

oscar-pistorius-6_2480644bMtaalamu wa mabomu aliyetoa ushahidi katika kesi inayomkabili Oscar Pistorius, alisema kuwa mwanariadha huyo hakuwa amevaa miguu yake bandia alipompiga risasi mpenzi wake Reeva Steenkamp nchini Afrika Kusini.

Ushahidi huu ulisikika katika kesi dhidi ya Pistorius inayoendelea Afrika Kusini.

Afisa huyo wa polisi alikuwa anatoa ushahidi wake kuhusu risasi zilizomuua marehemu Reeva Steenkamp.

Bwana Pistorius amekana madai ya kumuua mpenzi wake kwa maksudi wakati wa siku ya Valentine’s Day mwaka 2013 akisema kuwa alidhani alikuwa jambazi aliyekuwa amevamia nyumba yake.

Upande wa mashitaka unasema kuwa Oscar alimuua mpenzi wake kwa maksudi.

Katika siku ya 13 ya kesi hiyo, Kapteni Christian Mangena alisema kuwa, tathmini ya eneo ambapo mauaji yalifanyika, ilionyesha kwamba bwana Pistorius hakuwa amevalia miguu yake bandia alipompiga risasi Reeva.

Duru zinasema kuwa ni muhimu kujua ikiwa Pistorius alivalia miguu yake bandia au kwa sababu itasaidia upande wa utetezi kuonyesha kuwa mauaji hayo hayakuwa ya kupangwa.

Kapteni Mangena pia alisema kuwa japo hakuweza kubaini umbali alikokuwa Pistorius alipofyatua bunduki yake, hakuwa mbali na mita tatu kutoka katika bafu yake.

Inaarifiwa ushahidi huu unaambatana na utetezi wa Pistorius aliyesema kuwa alifyatua bunduki yake alipokuwa akisimama karibu na mlango wa bafu lake.

Alisema kuwa Reeva alianguka kabla ya risasi nyingine mbili kumgonga mkononi mwake na kichwani.

SOURCE: BBC

Tupia Comments