Habari za Mastaa

Baada ya story ya Chris Brown kuwa na mtoto, haya ni maneno 21 kwenye tweet ya Karrueche..

on

SPL821015_011

Mitandaoni jana na leo story kubwa kwa Marekani kuhusu mastaa ni ishu ya Chris Brown kuwa na tetesi ambazo zimegeuzwa ishu kubwa japo mwenyewe hajathibitisha  kuwa eti jamaa huyu ni baba wa mtoto wa kike mwenye umri wa miezi 9 sasa huenda ukawa mwisho wa mapenzi yake na mwanamitindo Karrueche Tran.

Chris Brown anadaiwa kuwa ana mtoto ambaye wamezaa na mwanamitindo Nia ambaye waliwahi kuwa na uhusiano ambao haukudumu kwa muda mrefu.

Karrueche ameandika kwenye ukurasa kwenye ukurasa wake Twitter jana kuwa hana mpango wa kuendelea na uhusiano na staa huyo huku akimtakia maisha mema na familia yake; “Listen. One can only take so much. The best of luck to Chris and his family. No baby drama for me“–@karrueche

Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook

Tupia Comments