Habari za Mastaa

Picha za Swizz beatz na Alicia keys huku Mashonda akishuhudia zimeleta huruma.

on

1Alicia Keys na mume wake Swizz Beatz pamoja na mke wake wa zamani Mashonda na watoto wao walikuwa kwenye mapumziko ya kifamilia ufukweni lakini watu hawakuwaza tena starehe zao bali kumuhurumia Mashonda pale Swizz alipombusu Alicia mbele ya Mashonda.

Zamani Mashonda aliwahi kumshtumu Alicia Keys kama muharibifu wa nyumba za watu baada ya kugundua kwamba anamuibia mume…. yaani  ‘Swizz’

Wawili hawa ambao inadaiwa walikua marafiki, hivi karibuni waliungana kwenye mapumziko ya kifamilia ambapo Mashonda akiwa na mtoto wake mmoja wa kiume aliezaa na Swizz Beats na Alicia Keys mke wa sasa ana mtoto mmoja pia anaitwa Egypt.

Mitandao kadhaa imeripoti kwamba labda maelewano mabaya kati ya Mashonda na wawili hao yamepungua hadi amekubali kuungana nao kwenye mapunziko hayo ya kifamilia.

2
3
4
5

Tupia Comments