Premier Bet
TMDA Ad

Michezo

Amunike amtema Ajibu na Mkude Taifa Stars

on

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Emmanuel Amunike ametangaza majina ya wachezaji 32 kati ya 39 watakaosafiri na Taifa Stars kuelekea nchini Misri katika maandalizi ya kambi ya mwisho kabla ya kuwachuja na kubaki 23.

Majina ya wachezaji 7 walioachwa ni pamoja na Shomari Kapombe aliyepata majeruhi, Ibrahim Ajibu wa Yanga, Jonas Mkude wa Simba, Ally Ally wa KMC, Kennedy Juma wa Singida United, Ayoub Lyanga wa Coastal Union na Kassim Khamis wa Kagera Sugar.

Taifa Stars wanaondoka leo kuelekea Misri watakapoweka kambi ya wiki mbili kabla ya wiki mbili kabla ya kuanza kwa fainali za AFCON 2019 ambapo wamepangwa Kundi C na timu za Algeria, Senegal na majirani Kenya.

Soma na hizi

Tupia Comments