Top Stories

Kijana alietengeneza pikipiki apelekwa VETA kusoma ufundi wa magari (+video)

on

Mkuu wa Chuo cha VETA Kigoma Saidi Ally amethibitisha kumpokea Zuberi Abdallah ambaye ni Mkazi wa Kigoma mwenye miaka 20 aliyeishia darasa la 6 ambaye alitengeneza pikipiki ndogo inayowaka na kutembea ambayo ina sifa za pikipiki kubwa.

Zuberi ataanza rasmi mafunzo ya ufundi umeme wa magari, akizungumza na AyoTV Mkuu wa Chuo hicho amesema kuwa gharama zote za masomo zitagharamiwa na VETA.

KIBAKA KALAZIMISHWA ANYWE LITA 40 ZA MAZIWA ALIYOIBA “SHIDA ZIMENIPONZA”

Soma na hizi

Tupia Comments