Habari za Mastaa

Watu wangu wa Kigoma,ipokeeni hii toka NMB bank.

on

DSC_0935Hii kwa watu wangu wa nguvu wa Kigoma Benki ya NMB imezindua rasmi tawi lake jipya mjini Kigoma ambapo Uzinduzi wa tawi hilo lililopo jengo la Bima barabara ya Lumumba ulifanyika katika jengo la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) mwishoni mwa wiki.

DSC_0967Tawi hilo lililo mkabala na Soko Kuu la Kigoma,limelenga kutoa huduma kwa watu binafsi na wakazi wengi wa maeneo hayo hususan wafanya biashara ndogo ndogo uzinduzi wa tawi hili ulizinduliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Bw. Ramadhani Maneno.

DSC_0891Mtu wangu wa nguvu wa Kigoma,tawi hili la Kigoma litakua likitoa huduma zote kuanzia kuweka na kutoa fedha,huduma za mikopo,malipo kwa taasisi kubwa zikiwemo za serikali na nyinginezo.

 

Tupia Comments