Leo January 13 2017 mkuu wa kitengo cha kupambana na kuzuia dawa za kulevya nchini, Mihayo Msikela ametaja mikoa 6 ambayo imekuwa ikiongoza kwa kilimo cha zao la bangi na kusema kuwa wataendesha msako kwa wanaolima na kuuza bangi. Mikoa aliyoitaja ni Arusha, Morogoro, Iringa, Pwani, Tanga na Mara.
Mikoa iliyotajwa kulima bangi kwa wingi nchini
1.Arusha 'Arumeru'
2.Morogoro
3.Iringa
4.Pwani
5.Tanga
6.Mara 'Tarime' pic.twitter.com/c1DlR3TkWR
— millardayo (@millardayo) January 13, 2017
Aidha jeshi la polisi Arusha limetoa taarifa ya Operesheni iliyofanywa kwenye mkoa huo, kamanda wa polisi Arusha Charles Mkumbo amesema operesheni hiyo wameifanya katika wilaya ya Arumeru na kufanikiwa kukamata magunia 58 ya bangi, mbegu kilo 210 za bangi pamoja na kuharibu hekari 31 za bangi wilayani Arumeru.
Polisi Arusha wamesema ndani ya siku mbili wamekamata magunia 58 ya bangi, mbegu kilo 210 na kuharibu hekari 31 za bangi wilayani Arumeru pic.twitter.com/ElNNzASw9h
— millardayo (@millardayo) January 13, 2017
VIDEO: Shuhuda akielezea ajali ya moto Airport DSM usiku wa Jan 12 2017, Bonyeza play hapa hini