AyoTV

VIDEO: Rais Magufuli alivyohoji gharama za ujenzi hospitali ya mkoa wa Simiyu

on

Leo January 11 2016 Rais Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, ameanza ziara ya siku mbili mkoani Simiyu ambapo amezungumza na wananchi katika mara baada ya kuweka jiwe la Msingi katika hospitali ya mkoa wa Simiyu.

Akizungumza na wananchi hao Rais Magufuli amehoji gharama za ujenzi wa Hospitali ya mkoa wa Simiyu ambapo ameutaka uongozi wa mkoa wa Simiyu, wizara ya ujenzi na wakala wa majengo nchini TBA kukaa na kurejea gharama za ujenzi wa Hospitali hiyo wa Bilioni 46 kuwa hauendani na hali halisi ya aina ya jengo linalotakiwa kujengwa.

Rais Magufuli ametoa Shilingi bilioni 10 ili kukamilisha ujenzi wa hospitali hiyo. Unaweza kubonyeza play hapa chini kutazama

AyoTVMAGAZETI: IMF yaeleza hali ya uchumi waTZ, Manusura wasimulia ajali ya Jahazi Tanga, Bonyeza play hapa chini 

Soma na hizi

Tupia Comments