Habari za Mastaa

Unadhani wasanii wa siku hizi wanahangaika kutoka kimuziki? Dj Khaled ana haya majibu… (Audio).

on

ccc2

Muziki wa siku hizi umebadilika sana, kuanzia namna ya kufanya muziki hadi mauzo yake hii ni kutokana na ukuaji mkubwa wa teknolojia, hata namna ya kupromote muziki umerahisishwa siku hizi, na nguvu ya ukuaji wa social media ndio imezidi kuutangaza muziki kwa urahisi zaidi.

ccc3

Lakini kwa baadhi ya wasanii kama Dj Khaled anaona kuwa wasanii wa siku hizi hawatumii nguvu sana kuutangaza muziki wao kwani mitandao inafanya kazi hiyo kwa naiba yao. Akiwa kwenye interview moja Dj Khaled alisema kuhustle kwa wasanii wa siku hizi sio kugumu kama wasanii wa zamani…

WEST HOLLYWOOD, CA - FEBRUARY 11:  Producer/artist DJ Khaled attends BMI's "How I Wrote That Song" at Key Club on February 11, 2012 in West Hollywood, California.  (Photo by David Livingston/WireImage) *** Local Caption *** DJ Khaled

>>> “wasanii wa siku hizi hawajaelimishwa vya kutosha kuhusu  ile nidhamu nzima ya hustle ya muziki, muziki wa sasa hivi umebadilika wasanii wa siku hizi wamekuja kwenye wakati ambao kila kitu kipo mezani… sio kama sisi tuliokuwepo wakati huo ambako kulikuwa hamna Instagram wala nini…” <<< Dj Khaled

ccc4

>>> “gemu ya muziki imebadilika siku hizi, watu hawataki kutoa album hawaoni umuhimu wa album…hawataki kuwa kwenye lebo za muziki…nakumbuka sisi kipindi hicho tulikuwa tuna huslte kuingia Bad Boy Entertainment, Def Jam na lebo kubwa kama hizo lakini siku hizi haiko hivyo… hata jinsi wanavyopata hela, hawahangaiki sana…wasanii wa siku hizi hawajalelewa kwenye ule mstari wa kuheshimu ile hustle, nawapenda lakini huo ndio ukweli.” <<< Dj Khaled.

Msikilize akielezea tofauti ya wasanii wa zamani na wa siku hizi hapa chini kwenye hii sauti.


Nitakutumia stori zote ukibonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Soma na hizi

Tupia Comments