Habari za Mastaa

Khloe Kadarshian afanya maamuzi ya kufuta maombi ya talaka kwa Lamar Odom… sababu?!

on

Kumekuwa na headlines nyingi baada ya mchezaji maarufu wa mpira wa kikapu Lamar Odom kufikishwa hospitali baada ya kukutwa hoi hajitambui… staa kutoka kwenye reality show ya Keeping up with The Kadarshians, Khloe Kardashian akaamua kuwa karibu na Lamar kwenye kipindi baada ya taarifa hiyo kumfikia.

Badaaye headlines zikabadilika tena na kwa mujibu wa mtandao wa TMZ wa MarekaniKhloe alifanya maamuzi ya kuachana na mpenzi wake wa sasa ili awe karibu zaidi na Lamar baada ya Lamar kumtamkia Khloe kuwa bado anampenda!

khole1

Khloe Kadarshian na mume wake Lamar Odom.

Stori ipoje leo?… kwa mujibu wa mtandao wa TMZ wa Marekani, Khloe Kadarshian kaamua kufuta kesi yake ya kuomba talaka kutoka kwa Lamar baada ya mchezaji huyo kuapa kuachana na madawa ya kulevya, ili kuipa ndoa yao nafasi ya pili na kwa mujibu wa mtandao huo Lamar alisema yeye na madawa ya kulevya basi kwani amenusurika kufa… akasisitiza kuwa anampenda sana Khloe.

khole3

Familia ya Khloe Kadarshian bado inaonekana kutokushawishika na maneno ya Lamar kwani inasemekana mchezaji huyo alishawahi kuomba msamaha wa namna hiyo lakini hakujirekebisha.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Soma na hizi

Tupia Comments