Michezo

Kauli ya kwanza ya Zidane baada ya kutambulishwa Real Madrid

on

Club ya Real Madrid leo imemtangaza rasmi kocha wao wa zamani Zinedine Zinade Zizzou kuwa ndio kocha wao mpya kwa mara nyingine tena, hiyo ikiwa ni miezi 9 imepita toka kocha huyo aamua kujiuzulu baada ya ushindi wa tatu mfululizo wa UEFA Champions League.

Zidane baada ya kutangazwa rasmi na kutambulishwa kuwa amesaini mkataba wa miaka mitatu na kuchukua nafasi ya  Santiago Solari, Zidane baada ya kujiuzulu nafasi yake ile alidaiwa kuwa ni kutaka kulinda heshima yake ya kuondoka katika club hiyo kwa heshima kwani angeendelea angeweza kuboronga ila mwenyewe ameweka wazi sababu za kurudi.

“Nimerudi kwa sababu Rais ameniita nina furaha kurudi lakini haya ni majukumu makubwa kwa sababu watu wengi wanaipenda hii club, tulishinda taji la Champions League msimu uliopita lakini tumelipoteza mapema na Kombe la Ligi pia mapema sana, najua nilikosea wapi msimu uliopita na  naenda kufanya kadri ya uwezo wangu kuhakikisha hii timu inafanya vizuri”>>>Zidane

Mwinyi Zahera alisababisha shabiki wa Yanga abet mke wake

Soma na hizi

Tupia Comments