Michezo

Simba SC hao nusu fainali, wanasubiriwa na Mbao FC

on

Mabingwa wa watetezi wa ligi Kuu Tanzania bara club ya SImba SC leo waliingia uwanjani kuwania taji la Sport Pesa Super Cup ambalo wamelikosa kwa miaka miwili mfululizo, Simba SC waliingia uwanjani leo kucheza mchezo wao wa mtoano dhidi ya AFC Leopards ya Kenya.

Simba katika mchezo wake huo wamefanikiwa kuwatoa AFC Leopards kwa kuwafunga kwa magoli 2-1, magoli ya Simba yalifungwa na Emanuel Okwi dakika ya 13 na Clotous Chama dakika ya 48 wakati goli pekee la AFC Leopards likifungwa na Oburu dakika ya 61.

Ushindi huo sasa unawapeleka Simba kucheza mchezo wa nusu fainali dhidi ya Mbao FC ambao wamewatoa Gor Mahia ya Kenya katika mchezo wa mapema, kwa kuwafunga kwa penati 4-3, hiyo ni baada ya dakika 90 kumalizika 1-1, timu zilizofuzu kucheza nusu fainali ya SportPesa Super Cup ni Simba SC, Mbao FC, Bandari FC na Kariobangi Sharks.

VIDEO: Mwalimu Kashasha kuhusu pasi ya Ajibu kwa Fei Toto “Locomotive faint”

Soma na hizi

Tupia Comments