Michezo

Barcelona imetoka sare Champions League Messi jukwaani, Pique akicheza game ya 100

on

UEFA Champions League round ya nne iliendelea usiku wa November 6 2018 kwa game nane kuchezwa katika viwanja mbalimbali, FC Barcelona walikuwa Italia kucheza dhidi ya Inter Milan lakini licha ya kusafiri na staa wao Lionel Messi aliyeripotiwa kuumia mkono siku kadhaa nyuma inaonekana hakuwa fiti asilimia 100 hivyo akawekwa nje na kocha wake Ernesto Valverde.

FC Barcelona ambao walikuwa wanaongoza Kundi lao lenye timu za Inter Milan, Tottenham Hotspurs na PSV Endhoven, hawakuwa na presha na wakati wa mchezo na kuhakikisha wanatawala mchezo huo kwa dakika zote 90 kama walivyofanya baada ya mechi wakawa wanaongoza hali ya umiliki wa mpira kwa asilimia 65 kwa 35 na kuondoka na point moja baada ya sare ya 1-1 katika uwanja wa Gueseppe Meazza.

Baada ya mchezo kuwa mgumu kwa dakik zaidi ya 80 kwa kushindwa kufungana kwa magoli, FC Barcelona walipata goli lao la kwanza dakika ya 83 kupitia kwa Malcon Filipe lakini dakika nne baadae Mauro Icardi akaisawazishia goli Inter Milan, hata hivyo mchezo huo umemfanya beki wa FC Barcelona Gerard Pique kufikisha jumla ya game zake 100 za Champions League kucheza na anakuwa mchezai wa 10 wa Hispania kufikisha game 100 Champions League.

Ushindi huo umeifanya FC Barcelona kuendelea kuongoza Kundi hilo kwa kuwa na jumla ya point 10 baada ya sare ya leo, wakifuatiwa na Inter Milan waliopo nafasi  ya pili kwa kuwa na point saba, Tottenham nafasi ya tatu kwa kuwa na point nne na PSV wanashika mkia wakiwa na  point moja na wameaga mashindano hayo wanasubiri kucheza game zao mbili za kukamilisha ratiba.

Matokeo ya game za Champions League November 6 2018.

Hakuna anayemkuta Samatta kwa sasa Jupiter Pro League 2018/19

Soma na hizi

Tupia Comments