Michezo

Inaelezwa haya ndio masharti 6 ya Zidane kwa Rais wa Real Madrid kabla ya kusaini

on

Kwa mujibu wa mtandao wa tribuna.com unaeleza kuwa kocha wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zidane ameamua kurudi kuifundisha Real Madrid tena, baada ya kujiuzulu miezi 9 iliyopita kufuatia ushindi wa mataji matatu mfululizo ya UEFA Champions League.

Zidane amerudi katika club hiyo na kusaini mkataba wa miaka mitatu na kumrithi Santiago Solari ambaye ameshindwa kufanya vizuri na timu hiyo ila imeelezwa kuwa kuna tetesi kuwa Zidane amekubali baada ya Rais wa Real Madrid Florentino Perez kukubali masharti sita ya Zidane.

Inaelezwa kuwa haya ndio masharti matano aliyoyataja Zidane kwa mujibu wa Tribuna.com

1- Apewe mamlaka kamili ya kui-control team

2- Kuuzwa kwa wachezaji katika timu yake sio kitu anachokitaka kukiona.

3- Marcelo na Isco hawauzwi

4- Neymar kununuliwa

5- James Rodriguez asirudi tena Real Madrid hayuko katika mipango yake (yupo kwa mkopo Bayern)

6- Ajaribu kumsaini Kylian Mbappe kutoka PSG

Mwinyi Zahera alisababisha shabiki wa Yanga abet mke wake

Soma na hizi

Tupia Comments