Mix

Bongo Star Search Season 10 2019, kama una kipaji hii inakuhusu

on

Bongo Star Search (BSS) ni kipindi cha kusaka vipaji kupitia Televisheni, Kipindi hiki kimelenga kumtafuta Muimbaji mahiri kupitia usaili utakaofanyika mikoa mitano hapa Tanzania, watazamaji pia watashiriki kwenye mashindano ya kumchagua mshindi kwa kupiga kura mtandaoni.

BSS 2019 inatoa fursa msimu huu wa 10 wa kutafuta vipaji mahiri vya vijana machachari wa Kitanzania wenye vipaji vya kuimba, Bongo Star Search Inawakaribisha wale wote wenye Vipaji kushiriki Usaili kwenye Mikoa husika na kwenye Mtandao kupitia App ya StarTimes ON.

Usahili utaanza September 28 katika Mikoa 5, 28 & 29 September – Arusha at the Fuzz-Pointzone Resort (Mianzini) 4 & 5 October – Mwanza Rock City Mall, 10 & 11 October – Mbeya (Mbeya City Pub & Lounge), 17 & 18 October – Dodoma (Royal Village Hotel) na 23, 24 & 25 – Dar es Salaam (National Museum).

BSS 2019 itakuwa na majaji wanne watakaotoa kura za NDIO au HAPANA kwa washiriki baada ya kuangalia umahiri wao wa kuimba ukipata Kura Tatu za NDIO moja kwa moja utakua umeshinda kuingia mchuano wa pili, Usaili wa Mtandaoni utafanyika kuanzia October 8 & 30. Kwa kushiriki unaweza ukajaza form kupitia Application ya StarTimes ON kisha weka Link kwenye YouTube, au Jirekodi kisha post Instagram na kuweka hashtag #bssonlineaudition2019 na @startimestz.

VIDEO: Mimi Mars: Ugomvi kila saa, kugombana, visa, kuachwa kwa sms, You Again? (+video)

Soma na hizi

Tupia Comments