Top Stories

Kichaa amuua Mtoto kwa kumgongesha kwenye gogo la mti

on

Mtoto Agnes Kiraba (3) mkazi wa kijiji cha Mtakuja kata ya Kirando wilayani Nkasi amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya wilaya hiyo baada ya kugongeshwa kichwa kwenye gogo na mtu anayesadikika kuwa ni mgonjwa wa akili.

Kamanda wa Polisi mkoani Rukwa, Justine Masejo amesema tukio hilo lilitokea January 3, saa 1:30 asubuhi, Mtoto huyo alikuwa anacheza nje ya nyumba yao pamoja na watoto wenzake, ndipo alipopita mtu huyo na kumkamata kisha kumgongesha kwenye gogo.

Baada ya tukio hilo Wazazi wa mtoto huyo walimkimbiza katika Kituo cha Afya Kirando kwa ajili ya matibabu lakini hali yake iliendelea kuwa mbaya hali iliyo lazimu kumpa rufaa na kumpeleka kwenye Hospitali ya Wilaya.

Alipofikishwa katika Hospitali hiyo alianza kupewa matibabu lakini alifariki dunia muda mfupi baadaye kutokana na kulalamika maumivu makali ya kichwa.

Kamanda Masejo amesema mtuhumiwa anashikiliwa na Polisi na atafikishwa Mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.

“HUYU SIO KICHAA, NAUONA UCHAWI, ANAOKOTA WATOTO BADALA YA MAKOPO” RC CHALAMILA

Soma na hizi

Tupia Comments