Asubuhi mapema ya leo April 13, 2017 kulizuka taarifa ambazo zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii zikieleza kifo cha Mwanasiasa mkongwe na Mbunge wa zamani wa Kwela ‘CCM’, Dkt. Crisant Mzindakaya.
Taarifa hizo zilieleza kuwa Dkt. Mzindakaya alifariki akiwa kwenye matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Dkt. Crisant Majiyatanga Mzindakaya, aliingia Bungeni kwa mara ya kwanza mwaka 1965 kama Mbunge wa Jimbo la Ufipa Kusini, lakini mbio zake ziliingia doa mwaka 1981 baada ya Mahakama kumvua Ubunge kutokana na ushindi wake wa mwaka 1980 kudaiwa kutumia faulu. Mwaka 1982 alirejea tena Bungeni baada ya kuteuliwa na Rais kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ambapo wakati huo wakuu wa mikoa walikuwa wanaingia Bungeni moja kwa moja.
Ayo TV na millardayo.com ilifika katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete na kumkuta mzee Mzindakaya akiwa mzima huku akiendelea vizuri ambapo kulikuwa na uwezokano wa kumruhusu.
Bonyeza play kutazama…