Miji/Nchi

Hotel 9 zenye mvuto zilizojengwa kwenye maji, Tanzania imo

on

Kila siku duniani kunafunguliwa Hoteli na sehemu za starehe zenye utofauti wa kipekee ambapo leo zimenifikia hizi Hotel tisa zilizotajwa kuwa na muonekano wa kipekee na mzuri zaidi na zikiwa zimejengwa ndani au juu ya bahari kwa mujibu wa CNN

Inawezekana kabisa kwa muonekano huu wapo ambao wataogopa kuchukua vyumba vya chini ya bahari lakini wamiliki wa hotel hizi wanasema huna haja ya kuwa na wasiwasi maana vioo vilivyotumika kwenye madirisha ni vigumu kwa kiasi cha kugongwa na kitu kizito mpaka kilo 150 na kisivunjike. 

Taj Lake Palace, Udaipur, India

Majengo ya hotel hii yalijengwa kama makazi ya Prince Maharana Jagat Singh II mwaka 1746, lilibadilishwa rasmi kuwa hotel mwaka 1970 na ndani yake kuna vyumba vya kulala 66 na master bedrooms 17 vyote vinatazamana na bahari.

Manta Resort, Tanzania

Tanzania pia imezichukua headlines kwenye list hii kwa kuingiza hotel moja iliyopo Pemba, Hotel hii inaitwa Manta Resort ambayo vyumba vyake vimejengwa chini ya bahari zaidi ya mita 250 kina ambacho kinafanya wateja kuona zaidi ya viumbe wa baharini 100 kila siku.

Inaelezwa kuwa gharama ya kupata chumba kimoja cha kulala ni dola 900 ambayo ni zaidi ya milioni mbili za Kitanzania kwa mtu mmoja kwenye usiku mmoja, watu wawili ni dola 1500 kwa usiku mmoja ambayo ni zaidi ya milioni 3 Tsh.

Good Hotel London, Uingereza

Conrad Maldives

Vyumba vya hotel hii vimejengwa kwa vioo vikiwa chini ya maji kwa urefu wa mita 5 na inapatikana kwenye visiwa vya Rangali ambako usafiri wake ni Boti tu au njia maalumu inayokufukisha kwenye hotel hiyo pekee, hairuhusiwi kama sio mteja kutumia njia hiyo, ilijengwa mwaka 2005.

Salt & Sill, Sweden

Salt & Sill: ina jumla ya vyumba 23 vya kulala, kuna umeme wa kujitegemea unaozalishwa kwa maji ya bahari hivyo hata umeme ukikatika eneo lote la Hotel linabakia na umeme wake.

Beach Villa Ocean Suites at Resorts World Sentosa, Singapore

Muonekano wa haraka kwenye hotel hii ni kama kila kitu kinaishia kwenye majengo ya juu lakini kuna sehemu mbili tofauti kwenye majengo haya, kuna eneo la juu ambalo ni kwa ajili ya biashara za maduka na sehemu nyingine za starehe wakati upande wa chini kwenye maji kumejengwa vyumba vya kulala wageni.

Inakadiriwa kuwa kuna zaidi ya aina 50,000 za viumbe wa baharini huonekana kwenye vyumba vya chini ya bahari huku kukiwa na huduma ya internet ya Wi-Fi bure kwa saa 24.

Salt & Water Catamarans, Serbia

Salt & Water hufahamika pia kama nyumba meli kwa jinsi ilivyojengwa, bado ujenzi unaendelea ingawa inatarajiwa kukamilika mwaka huu ambapo kila chumba kitakuwa kinajitegemea kwa kila kitu kuanzia sehemu ya mapokezi na sehemu ya vinywaji.

OFF Paris Seine, Ufaransa

OFF Paris Seine’s Sunset Suite: Ina muonekano mzuri kwa ndani ikiwa imewekewa fanicha za kisasa ambapo Hotel hii ina jumla ya vyumba 54 vya kulala ambapo kuna huduma ya chakula na vinywaji kwenye kila chumba.

Solent Forts, Uingereza

Solent Forts: Majengo yake yalijengwa karne ya 19 na yalitumika kama ngome ya majeshi ya Ufaransa wakati wa vita kuu ya pili ya duniani kabla ya kutelekezwa mwaka 1960 yalipobadilishwa kuwa hotel, kuna vyumba vya kulala zaidi ya 30.

Gharama za kulala usiku mmoja ni dola 1206 watu wawili ikiwa ni pamoja na huduma ya chakula na usafiri wa boti za kukufikisha nchini kavu. 
VIDEO: Tazama nyumba ya MILIONI 700 wanayoijenga Wasanii wa Tanzania Navy Kenzo Dar es salaam.

Soma na hizi

Tupia Comments