fB insta twitter

Baada ya Wizara ya Afya kuahirisha kutaja wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja TZ

on

Leo February 27 2017 Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ilikua na mpango kuwa na Mkutano na Waandishi wa habari ulioandaliwa kuwataja Watanzania wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja na kujiuza mitandaoni lakini baadae leo Mkutano huo uliahirishwa.

Baada ya kuahirishwa kwa mkutano huo, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla ameandika kupitia account yake ya twitter haya……

“Kwa orodha tuliyonayo, kutangaza majina ya mashoga hadharani, ni sawa na kufungulia jini lililowekwa kwenye chupa!”-Kigwangalla

“Kwa sababu za kimkakati, na ili kuepuka kuharibu ushahidi, tutalishughulikia jambo hili kwa namna nyingine, tutawajulisha matokeo kila hatua”-Kigwangalla

AyoTVMAGAZETI: Mawaziri 13 kikaangoni, Shein azushiwa jambo Zanzibar, Bonyeza play hapa chini kutazama 

Soma na hizi

Tupia Comments