Top Stories

Kigwangalla akubali yaishe “naomba radhi”

on

Mbunge wa Jimbo la Nzega mkoani Tabora ambaye pia ni mwanachama wa klabu ya Simba, Dr. Hamisi Kigwangalla amemuomba radhi mwekezaji wa klabu ya Simba, bilionea Mohammed Dewji kutokana na sintofahamu iliyotokea nyuma.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Kigwangalla amesema kuwa amekuwa akiwaza juu ya kusameheana na MO Dewji ili wasonge mbele, hivyo ametumia nafasi hiyo kuwaomba radhi mashabiki wa Simba pamoja na MO ili maisha yaendelee.

“Wanasimba tunataka ushindi dakika 90 uwanjani na mchango wa Mohammed siyo wa kudharau kwenye hili, lakini hata yeye na biashara zake wanafaidika na Simba ‘as a brand’, siyo bure tu. thamani ya Simba siyo majengo, ni brand yenye umri wa zaidi ya miaka 80” Kigwangalla.

“Nimekuwa nikiwaza juu ya kusameheana, yaishe tusonge mbele., naomba radhi kwake na kwa washabiki wote wa Simba niliowakwaza. Mimi nimesamehe. Maisha yaendelee”, Kigwangalla

ASKARI WA JESHI LA AKIBA WAJITOA KWA. AJILI YA WATANZANIA

Soma na hizi

Tupia Comments