Mix

Kazi ya kwanza kuifanya Naibu Waziri Kigwangala baada ya kuapishwa Dec 12 (+video).

on

Kwenye zama hizi za Hapa kazi tu za Mheshimiwa Rais John Magufuli,tunashuhudia mambo mengi ambayo mengine tulikua hatuyafikirii kama yanawezekana kufanyika kutoka kwa viongozi wetu,Dec 12 Mawaziri na Manaibu wao walioteuliwa na Rais Magufuli waliapishwa na baada ya kuapishwa wapo walioendelea na majukumu yao.

2Miongoni mwa Manaibu Waziri walioanza kazi yao mapema ni pamoja na Naibu Waziri wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Dokta Hamis Kigwangala baada ya kula kiapo alifanya ziara ya kushtukiza Dec 12 kwenye hospital ya Amana iliyopo Ilala Dar es salaam,nimenasa baadhi ya picha na video mtu wangu.

1Hii ni video alipoenda kwenye chumba cha Ultra Sound.

Tupia Comments