Jumanne Juma mwenye miaka 26 mkazi wa Mtaa wa Diskava, Kimara B, wilaya ya Ubungo DSM, ameuawa na watu aliokuwa akiwafanyia kazi za nyumbani kwa kumchoma na Petrol usiku wa Januari 23, 2024 wakidai amewaibia kiasi cha shilingi laki mbili.
Akiongea na AyoTV Mke wa marehemu Helen Mariki amesema watu waliomuua Mume wake walimfata nyumbaniusiku wakimtaka wakampe kazi nyingine na wakamlipe hela anayowadai wakaagiza mafuta ya Petrol kwa ajili ya kumchoma kwa sababu amewaibia.
Hosea ni jirani wa Jumanne nae anaelezea tukio lilivyokuwa usiku huo mpaka kuwakamata Watuhumiwa
Kwa upande wa Jeshi la Polisi tulipompigia Kamanda Muliro simu ilipokelewa na Msaidizi wake ambaye alitambia Tukio liko kwenye uchunguzi