Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda amemkabidhi Pikipiki mpya kijana Kusan Alex Dereva BodaBoda aliyesababisha ajali kwenye gari la Mkuu wa Mkoa October 31 2024, eneo la Chakechake Mkuyuni Jijini Mwanza.
Mtanda amebainisha kuwa kwa mujibu wa sheria za usalama Barabarani alikuwa na makosa lakini kama Kiongozi aliamua kumsaidia kwa kulipa gharama za matibabu kiasi cha Tsh. milioni 12, katika Hospitali ya Kanda ya Bugando, huku akieleza hatua hiyo inalenga
kumwezesha kijana huyo kurejea kwenye shughuli zake ili kusaidia familia yake.
Mkuu huyo wa Mkoa ameongeza kwa kusisitiza na kuwaomba vijana wanaojishughulisha na kazi ya BodaBoda kuzingatia sheria za Barabarani ili kuepusha ajali zinazoweza kuzuilika na kuhatarisha maisha yao.