Habari za Mastaa

Cardi B sasa kuonekana kwenye Filamu, aungana na Jeniffer Lopez

on

Rapper  Cardi B ametajwa kuwa miongoni mwa waigizaji watakaoshiriki kwenye filamu ya Jennifer Lopez  ‘Hustlers’ ambayo inahusu harakati na visasi vya wachojoaji (strippers) dhidi ya wateja wao wa kiume ndani ya klabu za usiku.

Kwa mujibu wa mtandao wa Deadline umetaja baadhi ya washiriki wengine watakaoshiriki kwenye filamu hiyo akiwemo Keke Palmer, Julia Stiles, Lili Reinhart na Mercedes Ruehl. Inatajwa kuwa Filamu hiyo imehamasishwa na makala iliyokuwa imeandikwa kwenye gazeti la New York mwaka 2016.

Inaripotiwa kuwa filamu ya ‘Hustlers’ inatarajiwa kuanza kurekodiwa March 22,2019. Jennifer Lopez na Cardi B wamewahi kufanya kazi pamoja kwenye ngoma ya Dinero akiwemo na Dj Khaled.

VIDEO: NOMA!! HII NDIYO LAST MINUTE YA IRENE UWOYA INABEBA WATU 300

 

Soma na hizi

Tupia Comments