Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akitembelea na kukagua mabanda ya wadau wa maendeleo katika Sekta ya Afya wanao shirikiana na Serikali pamoja na Taasisi ya Benjamini Mkapa katika utoaji wa huduma za Afya baada ya kuwasili kwenye Mkutano wa kumbukizi wa Hayati Mkapa unaofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar Es Salaam.
Rais Dkt Samia SuluhU Hassan ameambatana na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi pamoja na Mawaziri wa Serikali ya Tanzania na Zanzibar akiwemo Waziri wa Afya Tanzania Mhe. Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Mazrui pamoja na mgombea wa nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Kanda ya Afrika Dkt. Faustine Ndugulile.
Rais Dkt. Samia anatarajia kulifunga Kongamano hilo la kumbukizi la Rais Mstaafu Mhe. Benjamini Mkapa leo Julai 31, 2024 ambalo limewakutanisha wadau wa maendeleo katika Sekta ya Afya kutoka ndani na nje ya nchi ambapo pamoja na mambo mwngine walijadili juu ya mikakati na changamoto zinazoikabili Sekta ya Afya na namna ya kuzitatua.