Mix

Kilele cha Wiki ya huduma kwa mteja

on

Kampuni ya Emirates Aluminum imeadhimisha kilele cha wiki ya huduma kwa mteja kwa kukata keki na staaff wa kampuni yao kama ishara ya kushukuru wateja wao ambao wamekuwa wanao kwa kipindi chote.

Screen Shot 2020-10-10 at 7.10.23 PM.png

Afisa mahusiano wa Emirates Alluminium Issa Maeda ameelezea  kuwa kampuni yao itaendelea kuwa Bingwa wa kutoa huduma bora ili kukuwezesha mteja kuleta upekee katika nyumba yako.

Screen Shot 2020-10-10 at 7.22.43 PM.png

Kampuni ya Emirates Alluminium ni wauzaji wa vifaa vya ujenzi vya alluminium, kama vile milango, madirisha ya majumbani na ofisini ya kiwango cha ubora wakiwa na mawakala wao Tanzania nzima.

“Tumeamua kufanya hivi kwa ajili ya kukamilisha wiki ya huduma kwa wateja kama tunavyojua wiki ya kwanza ya mwezi wa 10 ilitengwa kuwa wiki ya huduma kwa wateja, tunapenda kuwakaribisha wale wateja wetu tunaofanya nao biashara na ma-agent tuendelee kushirikiana katika biashara tukiamini kuwa huu umoja ndio utawezesha tufanikiwe”>>> Gabriel Andrew aliyeongea kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu.

KOCHA BORA WA MWEZI WA VPL, MCHEZAJI BORA WA MWEZI ALLIANCE WAKABIDHIWA TUZO ZAO

Soma na hizi

Tupia Comments