AyoTV

VIDEO: ‘Lazima tukubali hapa tumefanya makosa’ –Devotha Minja

on

Mbunge wa viti maalum CHADEMA Devotha Minja alisimama bungeni Dodoma wakati akichangia bajeti ya Wizara ya Afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto kuhoji sababu za Serikali kutoa nafasi za ajira kwa madaktari 258 kati ya waliotaka kwenda kufanya kazi Kenya na kuwaacha wanaotafuta nafasi hizo za kufanya kazi nchini.

Devotha Minja amesema…>>>‘Leo hii sisi ndio wakupeleka madaktari wetu Kenya wakati wamesomeshwa kwa kodi za watanzani? Inabidi tukubali kuna mahali tumefanya makosa

Mimi najaribu kuwatazama wale ambao hawakujitokeza kwamaana pengine walikuwa na nia ya kutoa matibabu kwa watanzania lakini kitendo cha kuwaajiri madaktari 258 kati ya wale waliotahiniwa na kuwaacha wazalendo sio sawa’-Devotha Minja

Full video nimekuwekea hapa chini tayari…

VIDEO: Kipindi cha Maswali na Majibu Bungeni May 4, 2017 

BREAKING NEWS zote na stori za mastaa utazipata kwa Reporter wako MillardAyo, hakikisha umejiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter, Instagram, Snapchat, Youtube, APP kwenye ANDROID na IOS kote huko kwa jina hilohilo la @millardayo

Soma na hizi

Tupia Comments