Top Stories

Kilichobainika katika vita dhidi ya dawa za kulevya

on

Serikali kupitia tume ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, imekamata zaidi ya lita laki nne za kemikali ambazo ziliingizwa nchini pasipo kufuata utaratibu ambapo inadhaniwa kuwa hiyo ilikuwa mbinu ya uchepushaji wa kemikali hizo ili zikatumike kuzalisha dawa za kulevya.

Akizungumza na wanahabari wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupinga Matumizi ya Dawa za Kulevya; Waziri Jennister Mhagama, amesema baadhi ya kampuni zinazoingiza kemikali kutoka nje ya nchi zimebainika kuingiza nchini kemikali bashirifu ambazo hutumika katika utengenezaji wa dawa za kulevya.

LIVE: WAZIRI JENESTA MHAGAMA ANAZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI

Tupia Comments