Taasisi ya Green Growth Initiative ( GGI ) imepanda miti ya matunda na mbogamboga katika Shule ya Sekondari Taifa ikiwa ni hatua ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi yanayoleta athari kwa mazingira na viumbe hai.
Akizungumza Mara baada ya Zoezi la Upandaji leo jijini Dar es Salaama Mkurugenzi na Mwanzilishi wa GGI ,Thea Mosha amesema wamekuja na kauli mbili inayosema ‘Kesho yetu tunaanza kutengeneza kuanzia leo’ na wameanza na Wilaya ya Temeke kwasababu kuna wingi wa viwanda ambavyo vinazalisha kabondioksaidi ambazo zinaathari kubwa kwa jamii.
Huku Akisema shule ya sekondari Taifa inasifika kwa utunzaji mazingira wilayani humo kwahiyo wameanza kuotesha miti na zoezi hilo litakuwa endelevu huku lengo ni kuhakikisha wanafunzi kuanzia shule wajue namna gani ya kutunza mazingira.
Hata hivyo akamalizia kwa kuishauri serikali kuanzisha mashamba darasa mashuleni ili wanafunzi waweze kutumia siku za mwisho wa wiki kujitafutia kipato kwa kupitia kilimo Mosha ameeleza kuwa kupitia Miti hiyo pia watapata matunda na vivuli na pia ikikomaa wanapata mbao.