Michezo

Kilichoikuta Man United walipocheza na Swansea leo hiki hapa

on

(null)

Miezi takribani 7 tangu siku ya kwanza ya msimu wa 2014/15 wa ligi kuu ya Englang ulipoanza – ambapo tulishuhudia Swansea City wakimpa kipigo cha kwanza Louis Van Gaal katika uwanja wa Old Trafford – leo Kocha huyo kiholanzi alipata nafasi ya kurudisha kisasi.

Wakiwa nyumbani katika dimba la Liberty huko Cardiff City – Wales, Swansea wameweka rekodi nyingine kwa kuifunga Man United katika uwanja wao ikiwa ni mara ya kwanza tangu mwaka 1992.

Katika mchezo wa leo ambao United waliutawal kwa kiasi kikubwa – Ander Hererra alianza kuifungia goli Man United lakini kiungo Ki Sung Yeung na Bafetimbi Gomis wakaifungia magoli mawili Swansea na kuipa United kipigo cha 2 katika mechi 19 zilizopita.

Kwa matokeo hayo Man United imeshuka mpaka nafasi ya 4 kwenye msimamo wa ligi wakiwa na pointi 47.

Tupia Comments