Mix

Kilichoikuta Yanga leo dhidi ya Mtibwa Sugar na matokeo yote ya VPL haya haya

on

IMG_7371.JPG
Wiki moja baada ya kuifunga klabu bingwa ya Tanzania Bara Azam FC kwa magoli 3-0 kwenye mchezo wa ngao ya hisani, leo hii watoto wa Jangwani Dar Young Africans wamekutana na kisanga kizito kutoka kwa Mtibwa Sugar.

Katika mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Manungu mjini Morogoro umeisha kwa Yanga kutandikwa 2-0 na vijana wa Mecky Mexime.

Magoli ya Mtibwa yalifungwa na Mussa Hassan Mgosi katika dakika 15, kabla ya Ame Ally kuandika goli la pili dakika ya 82 ya mchezo huo.

Katika mchezo huo wa leo shujaa wa Yanga katika mechi dhidi ya Azam FC mbrazil Jaja alikosa penati.

Matokeo mengine kwenye ligi hiyo ni kama ifuatavyo: Stand 1-4 Ndanda, Azam 3-1 Polisi Moro, Prisons 2-0 Ruvu Shooting, Mgambo 1-0 Kagera, Mbeya City 0-0 JKT Ruvu

Tupia Comments