Top Stories

Kilichomkuta Mkuu wa Shule aliemdanganya Silinde, TAKUKURU waagizwa kuingilia kati (+video)

on

Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI David Silinde amemsimamisha kazi Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Tlawi iliyopo Wilaya ya Mbulu Mkoa wa Manyara na kuagiza uchunguzi ufanyike juu yake baada ya kumdanganya gharama za ununuzi wa cement na ujenzi wa bweni.

Hatua hiyo imekuja baada Silinde kufika katika Shule hiyo kufanya ukaguzi wa thamani ya fedha katika miradi ya lipa kwa matokeo ambapo kwa Shule ya Tlawi wao walipewa ujenzi wa madarasa matatu, bweni na choo kwa gharama ya Milioni 148.8 na kugundua kuwa fedha iliyotumika katika ununuaji wa vifaa ni nyingi tofauti na bei halisi.

Soma na hizi

Tupia Comments