Michezo

Kilimanjaro Stars imeendelea kuwa kibonde wa Uganda

on

Timu ya taifa ya Tanzania bara ambayo ni maarufu kwa jina la Kilimanjaro Stars imeendeleza unyonge dhidi ya Uganda kufuatia kupoteza katika mchezo wa nusu fainali.

Kilimanjaro Stars baada ya kumaliza nafasi ya pili Kundi B alicheza dhidi ya Uganda aliyemaliza namba 1 katika Kundi A katika michuano ya CECAFA Senior Challenge Cup 2019.

Matokeo hayakuwa mazuri kwa Tanzania bara baada ya kujikuta wakifungwa goli 1-0 lilifungwa na Fahad Bayo dakika ya 85 ya mchezo na kufanya huo kuwa mchezo wa 22 wa Tanzania bara dhidi ya Uganda katika CECAFA na kujikuta wakipoteza kwa mara ya 14 huku wakiwa wamewahi kushinda mara 3 na sare 5.

Soma na hizi

Tupia Comments