Top Stories

Kim azindua silaha nzito za kivita

on

Siku moja baada ya Korea Kaskazini kuandaa mkutano mkubwa wa kuadhimisha miaka 75 ya chama cha wafanyakazi kinachoongoza Nchini humo na kuonesha silaha mpya kubwa, Korea Kusini imefanya kikao cha dharura na kutoa taarifa ya kuikumbusha Korea Kaskazini kuhusu makubaliano yao ya kuzuia mapigano.

Ofisi ya Rais ya Korea Kusini imesema leo kuwa makubaliano kati ya Mataifa hayo mawili ya Korea ya kuzuia mashambulizi ya silaha na Korea Kaskazini lazima yaheshimiwe.

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un alitoa hotuba jana Jumamosi na kutoa wito wa ushirikiano mkubwa kati ya Mataifa hayo mawili pindi janga la corona litakapokamilika, lakini pia alitumia fursa hiyo kuzindua silaha mpya kubwa ambayo waangalizi wanaamini ni Kombora la Masafa Marefu lenye uwezo wa kutoka Bara moja kwenda Bara lingine.

Jeffrey Lewis, Profesa katika Taasisi ya mitaala ya Kimataifa ya Middlebury amesema kni dhahiri kwamba Kombora hilo linalenga kudhoofisha mfumo wa ulinzi wa makombora wa Marekani katika Jimbo la Alaska.

MOTO BADO UNAWAKA MLIMA KILIMANJARO “UMETUSHINDA, SHUGHULI ZA UTALII HAZIJADHURIKA”

Soma na hizi

Tupia Comments