Katika hatua inayosababisha wasiwasi mkubwa kwa jamii ya kimataifa, Kim Jong Un, kiongozi wa Korea Kaskazini, ametangaza nia yake ya kuongeza silaha za nyuklia baada ya kufanya ziara katika kituo cha siri cha uchakataji uranium ambapo hatua hiyo inaashiria kuongezeka kwa tishio la kimataifa kutoka kwa Korea Kaskazini, ambayo inaonekana kujiandaa kwa nguvu zaidi ya nyuklia.
Kim Jong Un, alionekana kuwa na furaha kubwa na kuridhishwa na maendeleo yaliyopatikana katika kituo hiki cha siri, huku akitoa maagizo ya kuongeza kwa kasi idadi ya silaha za nyuklia.
Ikiwa hii ni mara ya kwanza kwa Korea Kaskazini kutoa taarifa kuhusu kituo hiki cha uchakataji uranium tangu ilivyofunua Kituo cha Yongbyon kwa wanataaluma wa Marekani mwaka 2010, na kufanya hatua hii kuongeza hofu kuhusu maendeleo ya haraka ya nyuklia ya nchi hiyo.
Kiongozi huyo wa Korea Kaskazini, alionekana akitembea katika chumba cha kudhibiti na eneo la ujenzi litakaloongeza uwezo wa uzalishaji wa silaha za nyuklia, ambapo amesisitiza haja ya kuimarisha idadi silaha za nyuklia kwa ajili ya kujilinda dhidi ya vitisho vya kimataifa.
Na kulingana na Taarifa zinathibitisha kuwa Korea Kaskazini ina mashaka makubwa kuhusu tishio la nyuklia kutoka Marekani na washirika wake, na Kim ametoa onyo kali kuhusu uwezo wa kujihami na kushambulia mapema. Katika hali hii, tishio la nyuklia kutoka kwa Korea Kaskazini linaonekana kuwa la kweli na la hatari zaidi kuliko ilivyowahi kuwa hapo awali.