Top Stories

Kimbunga ‘Grace’ kupiga Haiti leo

on

Wakati majonzi yakiendelea kuwakumba Watu wa Haiti kufuatia kukumbwa na tetemeko kubwa la ardhi ambalo limesababisha vifo vya Watu 1,297 jana Jumapili, taarifa mpya kutoka Haiti ni kwamba leo usiku kunatarajiwa kuwa na Kimbunga.

Kimbunga hicho kilichopachikwa jina Grace kinatarajiwa kuipiga Haiti leo usiku, kikizidisha machungu ya wakaazi wa Nchi hiyo maskini.

Majanga haya yametokea wakati Nchi hiyo ikikumbwa na mzozo wa kisiasa kufuatiwa kuuawa kwa Rais wake, Jovenel Moise mwezi uliopita.

Waziri Mkuu Ariel Henry ametangaza hali ya dharura ya mwezi mzima na kuwataka Wahaiti kuonesha mshikamano.

KIJANA ATAJIRIKA KWA KUUZA UUME, KORODANI, NI MILIONEA “WANAWAKE WANAGOMBANIA, FREEMANSON KAWAIDA”

Soma na hizi

Tupia Comments