Habari za Mastaa

Kim Kadarshian anachukuliaje uamuzi wa Kanye West kugombea Urais? (Video).

on

Stori za Kanye West zimekuwa nyingi sana mara baada ya rapper huyo kutangaza kuwa ana mpango wa kugombea Urais kufikia mwaka 2020.. miongoni mwa watu walioshitushwa na habari hiyo ni mke wake Kim Kadarshian!

Akiwa anategemea kujifungua very soon, mke wa rapper Kanye West alipata time ya kwenda kufanya interview na Ellen DeGeneres kwenye kipindi chake cha The Ellen DeGeneres Show siku ya jumatano na kwenye show hiyo staa huyo aliongea vitu vingi kuhusu familia yake, baba yake aliyebadilisha jinsia pamoja na issue ya Kanye West kugombea urais wa Marekani mwaka 2020.

kimkaa

Kim Kadarshian kwenye Tv Show ya The Ellen DeGeneres Show.

Akiwa anahojiwa Kim Kadarshian alisema kuwa alishangazwa sana na kile alichokifanya mume wake kwenye usiku wa tuzo za MTV VMAs na kumbe Kanye hakuwahi kumwambia Kim kuwa ana ndoto za kugombea Urais na wala hakumshirikisha kwenye hiyo mipango!

kimkaa

Kim Kadarshian anategemea kujifungua mtoto wake wa pili ambaye atakuwa wa kiume tarehe 25 December.

>>> ” Taarifa ile kwangu ilikuwa kama breaking news, na hiyo topic haikuwahi kuwa discussion ndani ya nyumba yetu… na hicho ni kitu kikubwa sana kutokumshirikisha mke wako!” <<< Kim Kadarshian.

Licha ya kushitushwa na taarifa hiyo, Kim amesema kuwa atamsupport mume wake kama akiamua kweli kugombea Urais wa Marekani mwaka 2020“Naamini yupo serious, na najua akiweka akili yake kwenye kufanya kitu, atakifanya kadri ya uwezo wake… japo sijui kama alipanga ama aliibuka tu na hayo mawazo pale on stage.” alisema Kim Kadarshian.

kimkaa2

Ellen DeGeneres.

Wengi tunajua kuwa Kanye West ni mtu wa matani sana na akikerwa kidogo tu anafanya maamuzi ya hapohapo bila kufikiria sana na pengine hasira ikipungua yale aliosema yanakuwa yameshapita tayari… licha ya hayo Kim Kadarshian yupo tayari kabisa kuinga White House hata kesho!

Msikie mwenyewe anavyoelezea kwenye hiki kipande cha video hapa chini.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments