Kipigo cha Simba kwa wapinzani wao Yanga kimeibua vilio na taharuki kwa mashabiki wa timu hiyo ikiwemo kitendo cha mshambuliaji wake, Bernard Morrison kuondoka uwanjani.
Morrison alisusa na kuondoka uwanjani baada ya kufanyiwa mabadiliko “Sub” na kuingia Patrick Sibomana ikiwa ni kipindi cha pili baada ya kufungwa goli la 3.