Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un ametuma salamu za pongezi kwa Rais Vladimir Putin baada ya kusherehekea siku ya ushindi ya Urusi, akielezea mshikamano thabiti wa nchi yake na Urusi, shirika la habari la Korea Kaskazini KCNA limeripoti.
Katika barua yake iliyotumwa Urusi tarehe 9 Mei, Kim anasema “Mshikamano madhubuti wa muda mrefu kwa sababu ya Watu wa Urusi kung’oa vitisho vya kisiasa na kijeshi na usaliti wa vikosi vya adui”
Kim amesema imani yake ni kwamba uhusiano wa kimkakati na wa jadi wa urafiki kati ya nchi hizo mbili utakuwa kwa kasi”.
Hivi karibuni Korea Kaskazini imeangazia uhusiano wake wa karibu na Urusi, na kuunga mkono hadharani Urusi juu ya uvamizi wake nchini Ukraine, mwezi Februari, ililaumu mzozo wa Ukraine juu ya sera ya kivita ya Marekani na Magharibi.