Habari za Mastaa

Familia ya Kanye West kupokea ugeni mkubwa tarehe 25 December!

on

December ya mwaka huu itakuwa poa sana kwa familia ya Kanye West kwani mtoto wao wa pili anategemea kukaribishwa duniani tarehe 25 December, yani siku ya Christmas day mtoto North West atapokea ugeni mkubwa wa mdogo wake wa kiume!

kimye5

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ wa Marekani, Kim Kadarshian anategemea kujifungua siku ya Christmas yani tarehe 25 December na website hiyo inatuambia kuwa watu wa karibu wa familia ya Kim na Kanye wamekaa na madaktari na kuthibitisha kuwa mtoto wao wa kiume atazaliwa siku hiyo ya Christmas!

NEW YORK, NY - FEBRUARY 14: (L-R) Kim Kardashian, North West and Kanye West attend the Alexander Wang Fashion Show during Mercedes-Benz Fashion Week Fall 2015 at Pier 94 on February 14, 2015 in New York City. (Photo by Craig Barritt/Getty Images)

Kanye West, Kim Kadarshian na mtoto wao wa kike North West.

Mtandao wa TMZ umeendelea kuripoti kuwa familia hiyo tayari imeshaanza maandalizi kwa ajili ya ugeni wa mtoto wao wa kiume na tayari wameshabook hospitali ya Deluxe Maternity Suite & Medical Centre ambayo Kim Kadarshian ataenda kupata huduma ya kujifungua huko Los Angeles Marekani, hospitali ambayo mtoto wao wa kwanza North West alipozaliwa!

kimye4

Japo ya Mungu mengi na pengine mambo yanaweza kubadilika kutokana na hali ya Kim Kadarshian kubadilika mara kwa mara kipindi hiki kitu kinachowapa madaktari pamoja na mume wake Kanye West wasiwasi mkubwa lakini matumaini makubwa ya madaktari ni kuwa Kim atajifungua mtoto wake wa pili salama bila matatizo yoyote.

kimye6

Tunajua kuwa Kanye West anapenda sana kujiita ‘Yeezus’ jina ambalo tayari limekuwa sehemu ya brand yake na taarifa inasema kwamba mtoto wa pili wa Kanye atavuta pumzi yake ya kwanza tarehe 25 December mtu wangu… unahisi ataitwa nani? Jesus, Yeezus!? Share na mimi mawazo yako hapa chini kwenye comment!

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasamuziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata, pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>> YouTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments