fB insta twitter

Kanye West na Kim Kardashian kuwasaidia watoto 1000 msimu huu wa Christmas kwa mchango huu..!

on

Msimu huu wa Christmas 2015, Kim Kardashian anaziteka headlines kwenye pages mbalimbali za social media na websites za Marekani baada ya tweets zake kupitia page yake ya Twitter kugusa watu wengi.

Siku mbili zilizopita, Kim Kardashian alikuwa anatazama TV nyumbani kwake na ndipo alipokutana na stori ya msichana mmoja anayejaribu kukusanya pair 1000 za viatu ili kuwasaidia watoto wa shirikia la watoto yatima, Soles for Souls… shirika ambalo lilimsaidia msichana huyo kipindi cha mafuriko ya mvua za Katrina.

51398104 Reality star Kim Kardashian and tennis star Serena Williams go shopping at Lanvin together in Paris, France on April 30, 2014. Is Kim picking up a wedding dress? FameFlynet, Inc - Beverly Hills, CA, USA - +1 (818) 307-4813 RESTRICTIONS APPLY: USA ONLY

Baada ya kuguswa na stori hiyo, Kim Kardashian akaona itakuwa jambo zuri kwa familia yake kutoa mchango wao na ndipo alipoingia twitter na kuomba watu wamsaidie kumtafuta msichana huyo kwani yeye na Kanye wapo tayari kumsaidia kufanikisha lengo lake kwa kumpatia pair hizo… kupitia page yake ya twitter @KimKardashian, Kim alipost tweets kadhaa zilizosema…

Souls1>>> “Nimeamka kunyonyesha huku nikitazama kipindi hiki cha Dish Nation. Nimeisikia stori iliyonigusa ya msichana anayejaribu kukusanya pair 1000 za viatu…” <<< @KimKardashian.

Souls3>>> “Kanye na mimi tungependa kuchangia hizo pair 1000 kwa Souls For Souls“. <<< @KimKardashian.

Souls2>>> “Kuchangia kwa ajili ya Soles For Souls! Walimsaidia kipindi cha mafuriko ya mvua za Katrina. Nadhani namjua mbunifu wa Tuzo ya kiatu cha mwaka!” <<< @KimKardashian.

Souls4

>>> “Nimekuwa nikimtafuta huyu msichana online ili niweze kumwambia kuwa viatu vipo njiani… lakini nashindwa kumpata…” <<< @KimKardashian.

Souls5

>>> “Popote pale ulipo… hivi viatu ni kwa ajili yako! Tutawasiliana na Soles For Souls! Umetimiza lengo lako, so proud of you!!! xoxox” <<< @KimKardashian.

Souls6

>>> “Mnaweza mkanisaidia kumtafuta msichana anayejaribu kukusanya pair 1000 za viatu kufikia Christmas @DishNation @Soles4Souls, Kanye na mimi tungependa kuchangia!” <<< @KimKardashian.

Baada ya taarifa hii kusambaa kwa kasi kwenye mtandao wa Twitter, Twitter iliamua kumsaidia Kim kumpata msichana huyo ambaye jina lake ni Amelia Flores mwanafunzi wa sekondari ambaye shirika la Soles for Souls lilimsaidia yeye na familia yake baada ya mafuriko  ya Katrina na toka kipindi hicho msichana huyo amekuwa akijitoa mara kwa mara kulisaidia shirika hilo linalosaidia zaidi ya watoto milion 24-40 duniani.

Soles3

Adidas Yeezy Boost 350 (Black)

Safari hii Amelia alikuwa anajaribu kukusanya pair 2000 za viatu lakini kutokana na msaada wa Kim na Kanye msichana huyo ameshafikisha lengo lake kwa asilimia kubwa… na kwa upande wa viatu vilivyotolewa, Kim na Kanye wametoa pair 1000 za viatu kutoka toleo la Adidas Yeezy Boost 350 (moja ya collection za viatu vya Kanye West) miongoni mwa viatu vya bei ya juu kwa mwaka huu wa 2015.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FBInstagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments