Michezo

Kinda Azam FC asaini Maccabi Tel Aviv

on

Mchezaji wa Azam FC Novatus Dismas (18) aliyechini ya Shadaka Sports Management amesaini mkataba wa miaka mitatu na Bingwa wa Israel Maccabi Tel Aviv.

Dismas ambaye aliibuka mchezaji bora chipukizi wa Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2019/2020 ataanza kuwa chini ya Academy ya Maccabi Tel Aviv na baadae anatazamiwa kupandishwa.

Novatus Dismas ni kinda aliyelelewa na kukulia katika Academy ya Azam FC na msimu wa 2019/20 alitolewa kwa mkopo katika klabu ya Biashara kabla ya baadae kurejea Azam FC.

Soma na hizi

Tupia Comments