Michezo

Kinda Man City adaiwa kujiua baada ya kuachwa

on

Kinda wa Man City Jeremy Wisten (17) inadaiwa kuwa amejiua kutokana na msongo wa mawazo baada ya kuachwa na club hiyo.

Jeremy ni mzaliwa wa Malawi ambaye alihamia England na familia yake wakati akiwa bado mdogo na baadae kuanza maisha yake soka akiwa na Juniors FC na 2014 akajiunga na De la salle FC.

Mwaka 2016 Jeremy alisajiliwa na Man City katika kikosi cha U-13 na kuanza safari yake ya soka ambapo hakupata nafasi timu ya wakubwa, hata hivyo vyanzo baadhi vinaripoti kuwa mchezaji huyo kajiua huku wengine wakiripoti kifo chake pasipo kutaja sababu.

Soma na hizi

Tupia Comments