Mix

Ifahamu nchi ya kwanza duniani kuzima mitambo ya Radio za FM

on

Mwaka 2017, utakuwa wa kihistoria nchini Norway ambapo serikali imetangaza kuanza kuzima mitambo yote inayoendesha Radio za FM kuanzia wiki ijayo na kuhamia mfumo mwingine wa kisasa zaidi uitwao Digital Audio Broadcasting (DAB), na uzimaji utafanywa kwa awamu ambazo zitakamilika rasmi mwaka 2018.

Serikali ya Norway imesema inazima mitambo ya radio za FM na kuhamia kwenye mfumo wa utangazaji wa digital radio unaofahamika kama DAB utakaomuwezesha mzikilizaji kupata radio nyingi zaidi kuliko mfumo wa masafa (Frequency), na pia utaongeza ubora wa sauti za radio.

“Sababu kubwa ya kufanya hivyo japokuwa inakuwa nchi ya kwanza duniani ni kwamba Norway ina mazingira magumu sana kwenye kusafirisha mawimbi ya radio za FM kutokana na Jiografia yake, Norway ina mafuriko ya mara kwa mara, milima mirefu, pamoja na jamii zilizojitenga. Hii imekuwa ikiongeza gharama zaidi kwenye ujenzi wa mitambo ya FM ukilinganisha na nchi nyingine” – Serikali ya Norway.fmradio norwMaamuzi haya yanaifanya Norway kuwa nchi ya kwanza duniani kuufuta kabisa mfumo wa utangazaji wa radio za FM na kuhamia mfumo wa matangazo ya kidigitali, ikiwa ni maamuzi yaliyopitisha na bunge la nchi hiyo siku chache zilizopita.

Pamoja na kupitishwa sheria ya kuzima radio za FM nchini humo, umefanywa utafiti kuhusu jinsi wananchi walivyolipokea suuala hilo ambapo kwa mujibu wa kura zilizopigwa imeonesha kuwa 66% ya wananchi wameupinga uamuzi wa serikali kuzima mfumo wa FM, wakati 17% wamekubali.

Inaelezwa kuwa baada ya Norway kuzima mitambo ya FM, nchi nyingine zitakazofata ni pamoja na Switzerland ambayo imetangaza kuzima radio za FM ifikapo mwaka 2020, Uingereza na Denmark zimepanga kuhama mfumo huo pia. Nchi nyingi zinasubiri kitakachotokea baada ya Norway na endapo utakuwa mfumo rahisi na mzuri zaidi nyingi zimeonesha kuwa zitahamia mfumo.

Ikumbukwe hapa Tanzania ilitokea wakati Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilipotangaza kuzima mitambo ya analogy iliyokuwa inaendesha utangazaji wa Televisheni ambapo mpaka sasa ni nchi nzima imeshakamilisha mfumo huo na kuingia kwenye utangazaji wa Digital Visual Broadcasting (DVB)

VIDEO: Ulikosa kumsikiliza Waziri wa Habari, Nape Nnauye kuhusu Maisha ya Wasanii, sheria za hakimiliki zikoje? Bonyeza play hapa kusikiliza.

Soma na hizi

Tupia Comments