Habari za Mastaa

Rihanna anahusika kwenye beef ya Chris Brown na Soulja Boy

on

Takribani wiki moja sasa kumwekuwa na majibizano makali kati ya msataa wawili wa Muziki, Soulja Boy na Chris Brown kutoka Marekani na kuifanya kuwa beef ya kwanza kwenye game ya hip hop inayotrend zaidi tangu mwaka 2017 uanze.

Kwa mujibu wa source za taarifa kuhusu Beef ya Breezy na Soulja Boy zilieleza kuwa jamaa walitofautiana kisa Soulja ali-Like picha ya Karrueche Tran ambaye ni Ex wa Chris Brown, hiyo ikataja kumkera Breezy kiasi cha kuandika kwenye page ya Tran kwamba akimuona Soluja atampiga.

Dunia nzima ikaamini chanzo cha beef hiyo ni Karrueche kumbe sio hivyo. Ripoti mpya zinasema Soulja Boy amemwambia kocha wake ambaye ni bondia mstaafu Floyd Mayweather, kwamba ugomvi wake na Chris haujaanzia kwa Tran, ulianzia tangu enzi za Rihanna.

Soulja amedai kuwa Breezy anamchukia tangu mwaka 2009 kwasababu alimualika Rihanna kwenye show yake na hapo ndio ugomvi wao ulianza.

VIDEO: Ilikupita hii performance ya CHRIS BROWN kwenye Mombasa Rocks Music Festival? Nilikurekodia kila kitu. Tazama hapa chini

Soma na hizi

Tupia Comments