Habari za Mastaa

AUDIO: Kilichosababisha Ommy Dimpoz na meneja Mubenga watofautiane

on

Kupitia Interview iliyofanywa ndani ya XXL ya Clouds FM aamehojiw meneja Mubenga ambaye aliwahi kuwa meneja wa star mwimbaji Ommy Dimpoz na amefunguka juu ya sababu zilizopelekea kuachana kufanya kazi kama meneja wa mwimbaji huyo pamoja na taarifa zilizopo mtaani kwamba wana ugomvi wa kuchukuliana mwanamke.

Kwa mujibu wa Mubenga amesema kuwa sio kweli kwamba yeye alitoka kimapenzi na mwanamke wa Ommy Dimpoz isipokuwa kuna mambo ambayo Ommy Dimpoz alianza kuyafanya na hayakuwa kwenye makubaliano yao hivyo akaamua kukaa pembeni.

“Mimi mwenyewe sikutegemea kama ingefika siku nitaacha kufanya kazi na Ommy, kwasababu ni mtu ambaye nilimchukulia kama ndugu, ilifika wakati hadi watu waliokuwa hawaelewani naye mimi nilikuwa nasimama kumtetea, nilipambana mpaka hapo alipofika” – Meneja Mubenga

Msikilize kwenye FULL INTERVIEW hapa chini.

AUDIO: Ommy Dimpoz alizitaja sababu zilizowagombanisha na Diamond Platnumz. Bonyeza play hapa chini kusikiliza

Soma na hizi

Tupia Comments