Mix

Siku 16 kabla ya kuapishwa, haya ni maoni mapya ya Wamarekani kuhusu Donald Trump

on

Zikiwa zimebaki siku 16 kabla ya kuapishwa na kuingia IKULU ya White House kwa Rais mteule wa Marekani Donald Trump, imetoka ripoti ya utafiti wa maoni ya watu nchini humo uliofanywa na Kampuni ya Gallup umeonesha kuwa, ni 46% tu ya watu ambao wanaamini kuwa Donald Trump anaweza kutatua misukosuko ya kimataifa.

Utafiti huu umeonesha kuwa, zaidi ya 50% ya wamarekani wana mashaka juu ya uwezo wa Rais mteule Donald Trump katika kutatua migogoro ya kimataifa, kutumia nguvu ya kijeshi kwa busara, au kuepuka kashfa kubwa katika utawala wake, akilinganishwa na Marais waliopita.

Takwimu zinaonesha asilimia 70 ya wamarekani walikuwa na imani na Barack Obama, George W Bush na Bill Clinton katika maeneo hayo kabla yao kuingia madarakani.

Utafiti huo pia umeonesha maoni ya Wamarekani kama ifuatavyo.

47% Wanaamini kuwa Trump atatumia kwa busara nguvu za kijeshi

44% Wanaona anaweza kuzuia kashfa kubwa kutokea kwenye serikali yake.

60% Wameeleza imani yao kwa Trump katika kushirikiana kwa ufanisi na bunge.

59% Wanaamini atashughulikia vizuri uchumi.

55% Wanaona ataweza kulinda maslahi ya Marekani nje ya nchi akiwa Rais.

53% Wanaamini ataweza kusimamia ofisi ya ikulu ya Marekani asilimia.

Rais mteule wa Marekani, Donald Trump anatarajia kuapishwa rasmi na kuchukua madaraka ya Urais wa 45 wa Marekani January 20, 2017.

VIDEO: Wapo Watanzania wanaoishi Marekani na hawaamini kama Donald Trump atatekeleza kauli yake ya kuwaondoa wahamiaji wote nchini humo. Mtazame Mtanzania huyu anayeishi Marekani.

Soma na hizi

Tupia Comments