Leo January 5, 2017 Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imetoa taarifa yake kuhusu kinachoendelea kwenye mgogoro wa mipaka uliozuka miaka michache iliyopita baada ya Malawi kueleza kuwa inalimiliki Ziwa Nyasa lote.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mindi Kasiga Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Tanzania amesema kuwa Serikali inategemea kufanya mikutano ya Tume ya Kudumu ya Ushirikiano ambapo suala la mipaka litajadiliwa ili kufikia muafaka wa kidiplomasia na Malawi hivi karibuni.
“Mambo makubwa ambayo tutayazingatia kwenye mkutano huo ni pamoja na mgogoro wa Ziwa Nyasa ambao kwa sasa uko kwa wasuluhishi na tuliambiwa tusiongelee chochote kwasababu kama tukiuongelea itakuwa kama hatuhitaji muafaka wa mazungumzo ya usuluhishi” – Msemaji Wizara Mambo ya Nje (Tanzania)
Kufahamu kila kitu serikali imekisema, tazama video hapa chini.
VIDEO: Yapo hapa MAMBO MATANO yanayomleta Waziri wa Mambo ya Nje wa China nchini Tanzania, Tazama Video hii hapa chini.